Mvukizo/Evaporation-Upotevu wa maji usioonekana kwa macho. |
Mvukizo
au Evaporation kwa kingereza ni hali ya maji kubadilika na kuwa katika maada ya
gesi.. Ili hii kutokea ni lazima nishati nyingi na mgandamizo wa hewa uwepo, na
ndio maana mvukizo huwa mkubwa kwenye maeneo yenye joto kali.. Mvukizo
hurudisha sehemu ya maji iliyoshuka kama mvua moja kwa moja katika angahewa (atmosphere) kabla
hayajatumika kwa shughuli yoyote.
Mvukizo/Evaporation
inatokea kuanzia muda mchache baada ya mvua kukatika hadi kwa kipindi cha msimu
mzima (whole season). Kama ilivyo katika mvua, mvukizo pia hupimwa kwa kizio
cha milimita chini ya muda fulani kwa kutumia kifaa kiitwacho Evaporation pan.
Kivyovyote sehemu hii ya maji ya mvua hupotea bure. Japo kiasi cha maji haya
kinachopotea huwa hakifahamiki na wapanga miundombinu wengi (infrastructure planners). Mfao angalia picha ya kwanza juu hapo, ni eneo la wazi bila hata miti pembeni wala uoto kitu ambacho ni kosa kubwa.
Mfumo wa mzunguko wa maji (Hydrological cycle) |
Upotevu
huu wa maji huwa kwa mfumo wa mvuke (water vapour), na mvuke hauonekani kwa
macho ya kibinadamu (usiwaze ule mvuke kwenye sefuria unalopikia chakula baada
ya kufunua mfuniko, la hasha fikiria eneo pana kama bwawa) hivyo huunda kiwango
cha maji ambacho hupotea bila kujua (unseen loss of water). Kutokana na
hili, kiasi kikubwa cha maji hupotea katika mito,mabwawa, mitaro ya kugwia maji
nakadharika.
Tazama
mifano michache ya upotevu huu wa maji:
1.Fikiria
eneo lenye ukubwa wa eneo 10KM2, na mvukizo katika uso wa eneo (Evaporation
in vicinity of the reservoir) 5mm/siku.
Kiasi
cha maji kinachopotea kwa siku (vizio vimebadilishwa vyote kweme mita kwaajili
ya uzidishaji)
=
5x 10-3 x 10 x 106 M2
=50,000M3
Kiasi
hiki cha maji (mita za mraba 50,000) zinatosha kuhudumia kijiji chenye makazi (households)
300 kwa matmizi ya nyumbani (domestic water supply) kwa miaka sita (Lakini
kinapotea kwa siku moja)
Au
tazama mfano wa pili:
Fikiria
eneo lenye maji kwa ukubwa wa 2KM2, na mvukizo katika uso wa eneo (Evaporation
in vicinity of the reservoir) 5mm/siku.
Kiasi
cha maji kinachopotea kwa siku (vizio vimebadilishwa vyote kweme mita kwaajili
ya uzidishaji)
=
5x 10-3 x 2 x 106 M2
=10,000M3
Kiasi
hiki ch maji ni sawa na mvua au maji ya kumwagilia yenye kiwango cha milimita
100 kutumika katika shamba la hekta moja. Kwa lugha nyingine kiasi cha maji
kinachopotea katika eneo la kuhifadhia lenye ukubwa wa kilometa mbili za eneo
kwa siku moja kinatosha kutumika kumwagilia shamba lenye ukubwa wa hekta moja
kwa mwaka mzima.
Kwa
mifano hiyo miwili unaweza kupata picha ya haraka kiwango kikubwa cha maji
kinachopotea kwa njia hii.
Nini
kifanyike?
Mbinu
za kupunguza upotevu huu wa maji zipo nyingi. Hapa nakutajia mbinu mbili rahisi
kuzielewa
- Kwanza ni kuhifadhi maji katika miundombinu yenye kina kirefu kuliko eneo la juu ( greater depth than surface area). Hii inapunguza eneo la maji linalofikiwa na jua na upepo hivyo kupunguza mvukizo.
- Kupanda miti kuzunguka eneo ulilohifadhi maji kwa maana upepo pia huweza kuchangia mvukizo kwa kiwango fulani.
Kumbuka
njia za upoteve wa maji katika mabwawa ziko nyingi na kila moja na njia yake ya
kupunguza kwa maana sio rahisi kuthibiti kwa asilimia 100.
Tazama bwawa hili lilivyozungukwa na miti. Kwa njia hii mvukizo huwa kidogo sana na nirahisi kingo zake kutumika kama mazalia ya samaki na kuchochea uzalianaji wa ikolojia nyingine. |
Nakupongeza
kwa kujifunza na endapo unaswali juu ya mada hii waweza uliza kwa nia yoyote
uipendayo. Like page yetu facebook pia (Water Droplet Community-WADCo Tanzania)
kwa mada nyingine nyingi zinazohusu maji, umwagiliaji, udongo na mazingira. Naamini pia umeelewa kiswahili changu ambacho pengine baadhi ya maneno huwa rahisi kueleweka yakitumika kwa lugha ya kiingereza.
Eng
Herman Nguki (Irrigation & Water Resources)
0763
639 101/0679 639 101
Follow instagram @eng.ngukiwamalekela
Nakukumbusha kwa mada mbalimbali za vijana, jamii,mahusiano na imani tembelea www.ngukiherman.blogspot.com |